missing

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 31/08/2020Mtoto amebakwa mara mbili- Zanzibar

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA ZNZ) kinasikitishwa na taarifa iliyotoka hivi karibuni kuwa mtoto wa miaka 12 huko Mwanyanya, mkoa wa Mjini Magharib, Unguja amebakwa mara mbili ndani ya wiki mbili.

Kutokana na taarifa hiyo kupitia vyombo vya habari na wazazi wa mtoto huyo waliamua kumhamisha baada ya kufanyiwa ukatili wa kubakwa mara ya kwanza na kumpeleka Wete, mkoa wa kaskazini Pemba, ambako pia alikutana tena na ubakaji.

Wakati  TAMWA ZNZ ikiliomba jeshi la polisi kuharakakisha hatua za uchunguzi wa kesi hizi thakili,  inapenda pia kuwaomba  wazazi na walezi kuwa karibu zaidi na watoto wao kwa vipindi vyote ili kuwalinda na watu waovu.

Wazazi kuwa karibu na watoto kunatoa ulinzi mzuri kwa watoto hao na hivyo kuwanusuru kwa kiasi kikubwa kufanyiwa ukatili na watu waovu.

Pia ikiitokea bahati mbaya mtoto akifanyiwa ukatili, tunashauri pia wazazi kuwa karibu mara mbili zaidi na watoto ili kuwafariji na kuwafundisha mbinu za kujikinga zaidi dhidi ya vitendo viovu.

 

Kitendo cha kumhamisha mtoto aliyebakwa kutoka sehemu moja na kumpeleka eneo jengine bila ya uchunguzi na ulinzi wa kina kunaweza kupelekea mtoto akaharibikiwa zaidi kimwili, kifra na kimaisha.

 

Aidha TAMWA ZNZ inasikitishwa kuendelea kwa vitendo vya ubakaji nchini kote ambavyo vinashamiri kila siku na vinasababisha kuleta hofu na madhara ya kila hali kwa watu wanyonge hasa wanawake na watoto.

Kwa mujibu wa taarifa za mitandao ya kupambana na ukatili wa kijinsia Unguja na Pemba kwa kipindi cha miezi sita Januari hadi Juni, 2020 matukio 108 ya ukatili wa kijinsia yameripotiwa  katika shehia mbali mbali.

Kati ya matukio hayo, matukio 51 yameripotiwa kuwa ni vitendo vya ubakaji wa watoto chini ya miaka 18.

 

TAMWA, ZNZ inawapa pole wazazi na watoto waliokumbwa na kadhia hiyo na pia kuwaomba kutovunjika moyo katika kufuatilia kesi kwenye vyombo vya sheria mpaka dadika ya mwisho ili haki iweze kutendeka.

 

Dkt. Mzuri Issa

Mkurugenzi,

TAMWA Zanzibar

 

 

Contact us

TAMWA ZANZIBAR
P.O.Box 741,
TUNGUU ZANZIBAR
Phone: +255772378378
Email: info@tamwaznz.org

Get Our Latest News

To get our news updats please insert your email and subscribe


© Copyright 2020 Tanzania Media Women's Association. All Rights Reserved